• frank@frankpseth.com
 • +255 (0) 713 275 301

TIMIZA MALENGO YAKO YA MWAKA HUU

Ni jambo la kawaida kwa watu wengi kuweka maazimio ya mwaka pale mwaka mpya unapoanza. Swali ni je! Ukisha weka malengo yako unafuatilia kuangalia unayatimiza? Kumbuka, mwaka 2019 unaelekea kati kisha ukingoni.

Mambo Muhimu ya Kukuwezesha Kutimiza Malengo ya Mwaka:

 1. Andika malengo yako mahali ambapo utayaona mara kwa mara (Write down your resolutions – Dreaming stage).
 2. Panga muda wa kutimiza kila lengo (Set time farame).
 3. Andika mikakati ya kutimiza kila lengo (Write strategies).
 4. Weka viashiria vya kutazama kupima ukasi wa kutimia lengo moja moja (Set milestones).
 5. Fanya tathmini ya ufanisi wako jinsi unavyotimiza malengo yako (Evaluation – Execution stage).
 6. Kila baada ya angalau miezi mitatu rejea yale malengo yako ili kuyaboresha (Review/Refine your resolutions).
 7. Endelea kuandika malengo yako kadri unapata wazo jipya. Ukiweza kuandika mapema malengo ya mwaka ujao au hata miaka kadhaa mbele yako ni vyema zaidi kwa sababu utaendelea kuyatafakari na kuyaboresha kadri siku zinasogea (Keep on dreaming).
 8. Kila lengo linahitaji taarifa fulani. Hakikisha unaandika taarifa muhimu unazopata kwa kila lengo ikiwa ni pamoja na kuandika majina na namba za simu za watu unaowahitaji kutimiza malengo hayo. Jichagulie vitabu bora vya kusoma na ujipe malengo ya kumaliza vitabu hivyo kwa muda muafaka (Research).
 9. Anza kujenga mtandao kwa kuzingatia malengo unayotaka kufikia. Chagua marafiki kwa makini. Ikibidi, baadhi ya marafiki waepuke kabisa (Networking).
 10. Kila unapotimiza lengo jipongeze au toa shukrani maalumu kwa hatua hiyo ya mafanikio (Giving back/celebration/thank giving).

Pamoja na malengo BINAFSI, ipo fahari katika kuona MSAADA tunaotoa KUENDELEZA wengine. Naam, hiiyo ndio hasa maana ya KUFANIKIWA. Kama mafanikio yetu hayajalenga KUINUA wengine kwa namna yoyote, hutuna tofauti na MTI mkuu uliofyonza RUTUBA ya nchi bila kuzaa matunda yoyote! Kumbuka SHOKA liko kwenye shina la mti usiozaa! (LK. 13:6-9 SUV)

 Dr. Frank P. Seth